SUA ILIVYOSHIRIKI WIKI YA MAONESHO YA NANENANE 2024 KANDA YA MASHARIKI

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeshiriki kikamilifu katika  maonesho ya kilimo maarufu kama Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl Julius Kambarage Nyerere katika Manispaa ya Morogoro. Zaidi ya washiriki 74 kutoka Ndaki, Idara, Kurugenzi na Vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo walionesha bunifu zao.Pia miradi  na tafiti kadha wa kadha kutoka kwa watafiti wanataaluma na wanafunzi mbalimbali  nao wameshiriki katika maonesho hayo.

Maonesho hayo ya Nanenane kwa mwaka huu wa 2024 Kanda ya Mashariki yalifunguliwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt. Batilda, Buriani na kuhitimishwa tarehe 8 Agosti2024 naWaziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda.

Picha 1: Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Mizengo Pinda(Kulia) akiwa na  Mkuu wa Mkoa Wa Morogoro Mh.Adamu Malima(mwenye kofia) walipotembelea banda la SUA kwenye maonesho ya wakulima Nanenane 2024

Maonesho ya Nane nane kwa mwaka huu wa 2024 yalibebwa na kauli mbiu yenye ujumbe unaosema:“Tushiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi”.

 

Picha 2: Kamishina general wa Jeshi la Magereza. Jeremiah. Katungu akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa afya ya mimea na vipando alipotembelea banda la SUA kwenye maonesho ya Nanenane 2024 katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza Dkt Devotha Mosha.

 

Picha 3:Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Alexander Mnyeti akipata maelezo ya Zana bora za kilimo kwenye maenesho ya Nanenane 2024.Katika viwanja vya Mwl Julius Kambarage Nyerere-Morogoro

 

Picha 4: Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof.Raphael Chibunda akitoa maelekezo kwa wataalamu wa idara ya misitu na nyuki alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Nanenane 2024.
Picha 5:Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma.Prof.Maulid Mwatawala(kulia) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa afya ya mimea na vipando alipotembelea maonesho ya Nanenane 2024 

 

Picha 6:Mkurugenzi wa shahada za Uzamili,Mafunzo,Uhaulishaji wa Tekinolojia na Ushauri wa Kitaalamu Prof.Japhet Kashaigili akipata maelezo kutoka kwa Naibu mkuu wa kitengo cha sayansi za udongo na miamba Dkt Nakei alipotembelea maonesho ya Nanenane 2024.

 

Picha 7:Ufugaji bora wa Nguruwe pia ulitolewa kutoka kwa wataalamu wa SUA kwenye maonesho hayo ya Nanenane 2024

 

Picha 8:Mtaalamu wa Lishe na Afya ya Mlaji kutoka SUA akitoa maelezo juu ya ulaji sahihi kwa mdau alietembelea maonesho hayo ya Nanenane 2024

 

Picha 9:Mtaalamu kutoka idara ya kudhibiti viumbe hai waharibifu akitoa elimu kwa mdau alietembelea maonesho hayo.

 

Picha 10:Shule ya udereva wa kuendesha mitambo mbalimbali kwenye kilimo iliwakilishwa vyema na wataalamu wa shule kuu ya uhandishi na mitambo.

 

Picha 11:Wakiwa na nyuso za furaha baadhi ya washiriki wa maonesho ya Nanenane wakiwa katika picha ya pamoja na kikombe cha mshindi wa pili wa maonesho hayo kwa mwaka huu wa 2024

 

Picha 12: Kikombe cha Mshindi wa Pili SUA iliibuka mshindi wa pili katika maonesho hayo ya Nanenane 2024.