Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendelea (ICE) kinawatangazia Mafunzo ya Muda Mfupi (siku nne hadi tano) katika nyanja mbalimbali yatakayotolewa mwaka 2022.
Mafunzo hayo ni kama ifuatavyo: Uzalishaji na Utunzaji wa Malisho ya Mifugo; Utunzaji wa Udongo na Afya ya Udongo; Mafunzo ya Uzalishaji na Udhibiti wa Mende; Kilimo Biashara na Ujasiriamali; na Uzalishaji na Utunzaji wa Malisho ya Mifugo. Mafunzo mengine ni pamoja na Ufugaji wa Ng’ombe wa Maziwa, Udhibiti wa Viumbe-hai Waharibifu kwa kutumia Mfumo wa Vizuizi katika Mashamba ya Mpunga ya Umwagiliaji Maji, Ufugaji wa Kuku, Ufugaji wa Samaki, na Ufugaji wa Nyuki. Mafunzo mengine ya muda mfupi yanahusu Kilimo cha Bustani: Uoteshaji na Utunzaji wa Mboga na Matunda, Ufugaji wa Nguruwe, Usindikaji wa Juisi na Jemu, Mafunzo ya Ugani: Mbinu mpya na masuala mapya katika tasnia ya ugani, na Mafunzo ya Kujiandaa Kustaafu. Tumia fursa hii adhimu kwa kuchagua na kushiriki mafunzo yanayotolewa na ICE, SUA. Pata habari zaidi kuhusu mafunzo hayo ya muda mfupi kwa kufuatilia hapa chini:
BOFYA HAPA KUPAKUA ORODHA YA MAFUNZO YA MUDA MFUPI, ICE, SUA 2022
BOFYA HAPA KUPAKUA FOMU YA MAOMBI YA MAFUNZO YA MUDA MFUPI, ICE, SUA, 2022
Picha 1: Inaonesha sehemu ya kufugia vifaranga vya kuku (sehemu ya kuatamia) katika banda la mfugaji aliyepata mafunzo ya muda mfupi ICE, SUA.
Picha 2a: Mheshimiwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete (aliyevaa shati la bluu) alipotembelea shamba la mifugo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
Picha 2b: Mheshimiwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete (aliyevaa shati la bluu) alipotembelea shamba la mifugo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
Picha 3a: Moja ya mjasiriamali (Bi Rehema) aliyeshiriki mafunzo ya ufugaji wa samaki, ICE, SUA akimwonesha mshiriki mwenzake teknolojia ya kuzalisha vifaranga vya samaki
Picha 3b: Bwawa la samaki la wajasiriamali aliyeshiriki mafunzo ya ufugaji wa samaki ya ICE, SUA yaliyofanyika kwa kushirikiana, Chuo Kikuu cha Dodoma and Mongolo Enterprises yaliyofanyika Dodoma