-
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) kinatangaza kozi za muda mfupi katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufugaji, kilimo, malisho ya mifugo, kilimo biashara, usindikaji wa chakula cha binadamu, udhibiti wa viumbehai waharibifu na kujiandaa kustaafu zitakazotolewa hivi karibuni katika mwaka 2021:
Na | Aina ya mafunzo | Tarehe | Kitengo kinachoshirikiana na ICE | Walengwa | Idadi ya Wshiriki |
1 | Ufugaji wa Kuku | 16 – 19
Agosti, 2021 |
Ndaki ya Kilimo | Wakulima/Wajasiriamali | 20 – 30 |
2 | Ufugaji wa Samaki | 23 – 26
Agosti, 2021 |
Ndaki ya Kilimo | Wakulima/Wajasiriamali | 20 – 30 |
3 | Uzalishaji na Utunzaji wa Malisho ya Mifugo | Agosti 31 – Septemba 3, 2021 | Ndaki ya Kilimo
|
Wakulima/Wajasiriamali/Maafisa ugani/ Wahamasishaji wa maendeleo | 20 – 30 |
4 | Usindikaji wa juisi na jemu | 07 – 10 Septemba 2021 | Ndaki ya Kilimo | Wajasiriamali | 20 – 30 |
5 | Kilimo Biashara na Ujasiriamali | 14 – 17 Septemba, 2021 | Shule ya Kuu ya Uchumi Kilimo na Stadi za Biashara | Taasisi za Utafiti na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali/Wajasiriamali | 20 – 30 |
6 | Ufugaji wa Nyuki | 21-24 Septemba, 2021 | Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii | Wakulima, Wajasiriamali, NGOs, Maafisa Misitu, Wahamasishaji wa maendeleo, Taasisi zinazojishughulisha na hifadhi ya maliasili | 40 – 60 |
7 | Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu kwa Kutumia Mfumo wa Vizuizi katika Mashamba ya Mpunga ya Umwagiliaji Maji | 27 – 30 Septemba,
2021 |
Kituo cha SUA cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu | Wakulima/Maafisa ugani | 20 – 30 |
8 | Mafunzo ya Kilimo cha Bustani: Uoteshaji na Utunzaji wa Mboga na Matunda | 04 – 07 Octoba 2021 | Ndaki ya Kilimo | Wakulima na wajasiriamali | 20 – 30 |
9 | Mafunzo ya Kujiandaa Kustaafu | 25 – 29 Octoba, 2021 | Idara ya Raslimali Watu | Wafanyakazi wanaojiandaa kustaafu na waliostaafu hivi karibuni | 20 – 30 |
10 | Mafunzo ya Ugani: Mbinu mpya na masuala mapya katika tasnia ya ugani | 01 – 05 Novemba, 2021 | Ndaki ya Kilimo | Maafisa ugani na maafisa maendeleo ya jamii wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Maliasili na Utalii, na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs), n.k. | 40 – 60 |
Tangazo hili la kozi fupi linapatikana vilevile kwa lugha ya Kingereza kwa kubofya alama ya bendera katika ukurasa wa mbele wa tovuti ya ICE
EVENT INFO :
- Start Date:Agosti 16, 2021
- Start Time:08:30
- End Date:Novemba 5, 2021
- End Time:16:30
- Number of Participants:20-60
- Location:ICE, SUA
Morogoro