SUA ILIVYOSHIRIKI WIKI YA MAONESHO YA NANENANE 2024 KANDA YA MASHARIKI

Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kimeshiriki kikamilifu katika maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi yaliyofanyika kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa minne(4) (Morogoro,Pwani, Dar es salaam na Tanga).Maarufu kama maonesho ya  Nanenane. Kama ilivyokawaida tangu kuanzishwa kwake, maonyesho haya yanafanyika katika viwanja vya Mwl. Julius. K. Nyerere vilivyopo katika Manispaa ya Morogoro.

Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane ya Mwaka huu ni Tushiriki Kikamilifu Katika Kuchagua Viongozi Bora wa Serikali Za Mitaa Kwa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mifugo Na Uvuvi”.

Kauli mbiu hii ya mwaka huu wa 2024, imetumika kwa kipindi chote cha maonyesho hasa katika shughuli mbalimbali,kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi wao bora ambao watasogeza mbele sekta hii muhimu kwa uchumi wa Taifa letu. Umuhimu wa haya yote kwa lengo la kuleta uzalishaji endelevu wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi  kwa kutumia mbinu bora hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia yanchi.

Washiriki zaidi ya 74 wakiwemo watafiti kutoka Ndaki, Kurugenzi, Idara na Vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo waliweza kushiriki kikamilifu huku wakionesha bunifu zao mbalimbali zikiwemo teknolojia na ujuzi ambazo ni mazao ya tafiti mbalimbali. Pia wanafunzi wa SUA pamoja na wakulima kutoka Mkoa wa Morogoro walipata fursa ya kushiriki katika maonesho hayo.

Maonesho hayo ya Nanenane ya  mwaka huu (2024) yalifunguliwa rasmi tarehe 2 Agosti na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Buriani. Katika hotuba yake amekipongeza Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA hwa matokeo Chanya ya Utafiti ambayo yatasaidia kuboresha sekta hii mama ya kilimo, mifugo na uvuvi. Pia Mh. Dkt. Batilda Buriani amefurahishwa sana na ushiriki wa wanafunzi wa SUA katika utafiti ambao umewaletea matokeo mazuri wanafunzi wa SUA na kuweza kuzalisha mazao mbalimbali ya kibiashara hivyo kujiongezea kipato kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao munimu.

Dkt. Buriani Awapongeza SUA kwa Tafiti za Kilimo,Mifugo na Uvuvi

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani akifungua wiki ya maonesho ya Nanenane 2024,kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl Julius. K.Nyerere manispaa ya Morogoro.

Maonyesho hayo yamefungwa rasmi tarehe 8 Agosti 2024 na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda.

Waziri Mkuu mstaafu Mh.Mizengo Pinda akikabidhi zawadi ya kikombe cha mshindi wa pili wa maonesho ya Nanenane 2024.Anayepokea zawadi hiyo ni Naibu wa Makamu wa mkuu wa chuo upande wa mipango,fedha na utawala.Prof .Amandus Muhairwa kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza(ICE).Dkt Devotha. Mosha.

 

PICHA MBALIMBALI NA MATUKIO KWENYE WIKI YA MAONESHO YA NANENANE 2024,VIWANJA VYA MWL JULIUS K NYERERE MANISPAA YA MOROGORO.

 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Adamu Malima,kushoto mwenye tai ni Kaimu Naibu wa makamu wa mkuu wa chuo Taaluma.Prof Samweli Kabote alipotembelea maonesho ya Nanenane 2024.

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Alexander Mnyeti(Mb), akipata maelezo ya zana bora za kilimo kwenye maonesho ya Nanenane 2024,kanda ya mashariki.

 

Makamu wa Mkuu wa Chuo.Prof Raphael. Chibunda akitoa maelekezo kwa wataalamu wa idara ya misitu alipotembelea maonesho ya Nanenane 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE).Dkt. Devotha. Mosha akitoa maelezo pamoja na kuwakaribisha wadau wote kwenye maonesho ya Nanenane 2024.

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda alipotembelea na kupata maelezo kutoka kwa wataalamu idara ya  misitu na nyuki. 

Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya St Mary Kihonda, wakiingia kwenye banda la SUA kwenye maonesho ya Nanenane 2024.

Vipando vya Mazao ya mbogamboga(kabeji) viliwavutia wadau wengi na kuja kwa kupata Elimu.

Mtaalamu wa idara ya Lishe na Afya ya mlaji akitoa elimu kwa mdau aliyetembelea maonesho ya Nanenane 2024.

 

Vipando vya majani ya malisho (Super Napier) Viliwavutia wadau wengi kutaka kujifunza upandaji bora wa malisho ya mifugo.

Utengenezaji na Uhifadhi Bora wa Majani makavu(HAY) uliwavutia wadau wengi wa ufugaji hasa nyakati hizi za mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi wa shahada za uzamili,tafiti,uhaulishaji wa tekinolojia na ushauri wa kitaalamu.Prof. Japhet Kashaigili akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa sayansi za udongo na miamba Dkt Nakei.

 

 

English version

SUA Participates in the Nanenane Agricultural Exhibitions 2024 in the Eastern Zone

Sokoine University of Agriculture (SUA) actively participated in the renowned agricultural exhibitions, commonly known as Nanenane. This year the exhibitions took place from 1st to 8th August 2024 at the Mwl. Julius Kambarage Nyerere grounds in Morogoro Municipality. The Eastern Zone Nanenane Exhibitions draw exhibitors from four regions of Dar es Salaam, Pwani, Morogoro and Tanga. This year’s theme:  “Let us actively participate in electing competent local government leaders for transforming agriculture, livestock and fisheries sub-sectors.” The theme resonated throughout the activities, displays and presentation and discussions highlighting the need for innovation and sustainable agricultural practices, especially under coping with climate change and variability.

More than 74 exhibitions from various SUA Units including Colleges, Directorates, and Departments had opportunities to showcase different products and innovations, which are outcomes of research projects. In addition, researchers, students and farmers actively participated in this year’s exhibitions.

The event was officially inaugurated by the Honourable Regional Commissioner of Tanga, Dr. Batilda Buriani, who generally appreciates the technologies, products and innovation outcomes from SUA research activities. The Nanenane exhibitions were officially closed in 8th August 2024 by Former Prime Minister, Honourable Mizengo Peter Kayanza Pinda.