Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dr. Leonard Akwilapo amepongeza jitihada zinazofanywa na Uongozi wa Chuo kikuu cha sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na serikali katika kuboresha miondombinu chuoni hapo.
Katibu mkuu huyo ameyesema hayo wakati akikagua jingo jipya la kulia chakula wananfunzi na wafanyakazi wa chuo linalojengwa kwa fedha za serikali kupitia wizara hiyo pamoja na miundombinu ya umwagiliaji inayojengwa kwaajili ya kuwezesha upatikanaji wa maji ya kumwagilia bustani na mashamba ya chuo kama sehemu ya kufundishia wanafunzi na wakulima nchini.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa chuo Prof. Raphael Chibunda ameishukuru wizara kwa fedha hizo na kumhakikishia kuwa ujenzi wa jingo la kulia wanafunzi litakuwa tayari kabla ya mwezi wa sita mwaka huu ili kurahisisha wanafunzi kupata sehemu nzuri na ya kisasa kwaajili ya chakula.
Prof. Chibunda pia amemwambia Katibu mkuu huyo kuwa wameamua kujenga bwawa kubwa ambalo litahifadhi maji mengi cha zaidia ya lita za ujazo milioni 4 kwaajili ya kusaidia umwagiliaji wa bunstani na mashamba ya maonyesho ya chuo mwaka mzima sambamba na kuchimba kisima kirefu cha mita mita 100 ili kusaidia shughuli hiyo. Ili kukifanya chuo hicho cha kilimo kiweze kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa na bustani nzuri,mashamba ya mfano kwaajili ya kufundishia wanafunzi na wakulima kutoka maeneo yote nchini.