ICE yapongezwa kwa kuandaa warsha kuhusu kuratibu shughuli za ugani

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE, SUA Dkt. Devotha Mosha akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kuratibu Shughuli za Ugani
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE, SUA Dkt. Devotha Mosha (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kuratibu Shughuli za Ugani

Wajumbe wa Kamati ya Kuratibu Shughuli za Ugani zinazotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) University-wide Outreach Committee (UWOC) wameishukuru Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza – ICE kwa kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakisema yatakuwa chachu ya kuratibu shughuli za ugani zinazoendelea kwenye kila eneo hapa chuoni.

Akifungua warsha hiyo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Giraffe uliopo ICE ikiwa na lengo la kubuni mfumo bora wa kuratibu shughuli za ugani SUA, Mkurugenzi wa ICE, Dkt. Devotha B. Mosha amesisitiza umuhimu wa wanawarsha kushiriki kikamilifu katika kutekeleza yale yote yatakayojadiliwa katika warsha hiyo katika kutekeleza majukumu yao ya kuratibu shughuli za ugani zinazotekelezwa na SUA kutoka kwenye Taasisi, Ndaki, Kurugenzi, Shule Kuu, au Idara na Vitengo wanazoziwakilisha.

“Mimi niwahimize wajumbe kila mmoja ashiriki kwenye hii warsha kwa kutoa mchango wake katika namna bora ya kuboresha shughuli za ugani ambazo kwa kweli ni muhimu sana kwa Chuo katika kuwafikia wadau wetu”, alisema Dkt. Devotha Mosha.

Mwezeshaji wa mafunzo ya kuratibu shughuli za ugani Dkt. Rwambali akitoa mada wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Giraffe ICE, SUA.

Akihitimisha warsha hiyo, mwezeshaji mkuu wa warsha Dkt. Emmanuel Rwambali amewataka wajumbe wakati wa ua ndaaji wa taarifa za kutofautisha kati ya majukumu ya ugani ya Chuo na ambayo hayahusiani na ugani ili ripoti zinazijadiliwa ziwe na tija kwa jamii kupitia maarifa na ujuzi unaotolewa na wataalamu kutoka SUA.

Dkt. Emmanuel T. Malisa, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Ugani (Outreach Section), ICE, akiongea katika warsha hiyo amesema wanategemea mafunzo hayo yatasaidia katika kuongeza ubora kwenye uandaaji na uwasilishaji wa ripoti ambazo zinawakilishwa kila baada ya miezi mitatu.

Matukio katika picha wakati wa warsha hiyo hizi hapa:-