Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza ICE kwa niaba ya chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) kupitia mradi wa Elimu ya juu kwa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) iliendesha mafunzo ya muda mfupi ya siku nne(4) kwa wajasiliamali na wafugaji juu ya ufugaji wenye tija wa kuku.Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 29/01/2024 hadi tarehe 01/02/2024 katika ukumbi wa Girrafe Hall uliopo hapa ICE-SUA ambapo zaidi ya wahitimu 42 kutoka zaidi ya mikoa nane(8) ambayo ni Morogoro,Dodoma,Pwani,Iringa,Dar es Salaam,Tanga,Kilimanjaro na Mwanza.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof Maulid Mwatawala akitoa neno kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku
Akifungua mafunzo hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma.Prof Maulid Mwatawala aliwaasa washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale yote yatakayofundishwa na watoa mada walio bobea katika tasnia ya kuku hapa inchini mojawapo akiwa Prof.Faustine Lekule alisema mbinu bora na za kisasa za ufugaji wa kuku zitawafanya washiriki kupata mabadiliko chanya katika ufugaji wao ambapo utakuwa ufugaji wa faida.
Mafunzo hayo yaligawanyika katika sehemu kuu mbili ambapo wanafunzi walikaa darasani(theory session)na pia walienda nje ya chuo kwa ajiri ya vitendo(practical) sehemu walizotembelea kwa ajiri ya mafunzo kwa njia ya vitendo ni pamoja na Modecco katika kiwanda cha TANFEED LTD na pia walitembelea eneo la mkambarani kujionea wafugaji wenzao wanavyofuga kuku.