Wahitimu wa kozi ya mafunzo ya ufugaji bora wa samaki wamekipongeza chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo(SUA) kwa juhudi zake za kutoa mafunzo yenye tija kwa jamii akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake Bw.Emmanuel Lyaruu amesema tunatoa pongezi zetu nyingi kwa wakufunzi wetu na uongozi mzima wa Chuo hiki kwa kutupatia mafunzo haya ya ufugaji wa samaki.Ni matumaini yetu ya kuwa elimu hii tuliyoipata hapa SUA tutaipeleka majumbani kwetu na kwenda kuifanyia kazi.
Mafunzo hayo ya ufugaji Bora wa Samaki yameratibiwa na Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE kwa niaba ya chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA).Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza/Institute of Continuing Education(ICE) kupitia kitengo cha Outreach imeendelea kutoa huduma Bora kwa Jamii kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi wahitaji wa aina tofauti iwe katika ufugaji/kilimo/ujasiliamali/mazingira nk